Lugha
Lugha
Lugha
Safari ya Vipepeo
Kuwa sehemu ya harakati iliyo buniwa kuandaa wafuasi wa Kristo miongoni mwa wale hawajafikiwa katika mataifa ya ulimwengu. Kama kipepeo lipeperukavyo kwa kasi, kupitia umbali mkubwa, na kuchavusha kila ua analoligusa, ni maombi yetu kwamba waumini watawaiga na kueneza Injili popote wanapoenda.
Tuna amini kwamba Live School ni chombo maalum iliyo na sifa ya kupanda makanisa ambayo yanadumu. Kwa kutumia chombo hiki cha kufaa kwa tamaduni tofauti, na lengo ya kuandaa wanafunzi katika nchi mbali mbali kwa zaidi ya miezi 6-18, tunataka kuona wamishenari milioni moja wameandaliwa duniani kote ifikapo mwaka wa 2030. Tunamwamini Mungu kwa hatua kubwa na kasi, kwa sababu, wakati ni sasa. Mavuno ni mengi na kuna haja ya dharura kwetu kama Wakristo kuwajibika na kuchukua hatua.
Iwapo maono haya yanagusa moyo wako, jiunge nasi. Kuwa sehemu ya harakati.
Soma Zaidi hapa chini au usajili hapo juu
“Inasisimua sana kuona kwamba, baada ya yote chombo hiki kinaingia mikononi mwa watu. Naona kwamba itaenea kote Amerika ya Kati.”
“Mtaala kwa muundo wa video, uliojumuishwa haswa kwa mpango wa upandaji makanisa, kuzidisha na mafunzo ya uongozi na ni bora hasa katika mazingira yetu ya mashambani ambako makanisa yanapanuka.”
“Asilimia 70 ya wahitimu wetu wamekwenda vijijini kupanda makanisa.”
“Kazi kuu ya makanisa yote ni; jinsi ya kuhamasisha watu kwa ajili ya huduma. Live School ni suluhisho nzuri sana kwa hilo.”
Bettie
Mishenari, Guatemala
Alok
Mchungaji nchini India
Felix
Mchungaji nchini Zambia
Duman
Mchungaji huko Kazakhstan
Kuna mambo kadhaa unapaswa kuzingatia na kuamua kabla ya kuanza ratiba ya Live School. Ni kama yafuatavyo:
Kabla ya kutazama
1) Shule inaweza kufanyika “kwa mfululizo” au “ kwa muda”
-
- Katika shule ya mfululizo utahitajika kupitia vipindi vitatu kila siku, hii itachukua wiki 18 kukamilisha.
- Katika shule ya muda utahitajij miezi 18. Unaweza kuamua jinsi ya kupanga mtaala katika kipindi hiki.
- Njia bora ya kuendesha shule ni kukusanya pamoja kundi la wanafunzi, familia au marafiki ili wajiunge. Kwa njia hii utasaidia kufunza watu wengi zaidi kuwafikia waliopotea. Hata hivyo, umekaribishwa kusoma mtaala huu pekee yako, haswa kama unaishi kwenye nchi yenye uhasama au vikwazo.
- Kama una kundi, tafadhali uliza kila mmoja wao kujiandikisha kwenye portal ya Live School ili tuweze kudhibiti maendeleo yao.
- Ni bora kuwa na muda maalum uliotengwa wa Live School ili kila mmoja awe nayo kwenye ratiba yao.
- Njia nyingine ni kila moja wa kundi lako kutazama vipindi vya video kibinafsi, kwa kasi yao wenyewe na hatimaye kujadiliana pamoja.
Unapotazama
2) Mara kundi wakiwa wote pamoja, kuwa na wakati wa maombi na kisha onyesha/watazame video. (Ni muhimu kutazama kozi na vipindi kwa mpangilio uliowekwa diski mweko (thumb drive) kwa sababu maadili ya Live School hujijenga kanuni hadi kanuni, ambayo huchangia sana maendeleo ya mwanafunzi.
-
- Wakati unapotazama kipindi cha video, andika kile kilicho cha muhimu au kipepee kwako.
- Kipindi cha video kinapokamilika, uwe na muda majadiliano na kutafakari juu ya kile kila mmoja amejifunza. Himiza kila mmoja kuongeza pointi yoyote huenda walikosa katika maandishi yao.
- Unapoenda nyumbani, tumia maandishi yako, andika ukurasa moja wa kutafakari kwa mfumo wa mahubiri (katika pointi za viaridhishi/ufupisho)
- Kisha pakia ukurasa wako moja wa maandishi kwenye portal yako kwenye tovuti yetu. Unaweza kupiga picha kupakia. Kwa hivyo, hakuna haja ya kuitambaza.
- Weka maandishi yako ya ukurasa moja kwenye faili kama kumbukumbu na kwa matumizi ya baadaye.
- Endelea na mchakato huu hadi utakapokamilisha kozi.
Pindi unapokamilisha vipindi vyote vya Live School
3) Cheti cha ukamilisho wa Live School hutolewa baada ya maagizo haya kutimizwa:
-
- Umesoma na kukamilisha mtaala yote (masaa 242).
- Umepakia kurasa moja moja za maandishi kwenye portal yako.
- Umetuma ombi la cheti kwa kuenda kwa tovuti yetu na ukabonyeza kwenye “Ombi la Cheti cha Ukamilisho.”
4) Ikiwa unakusudia kuendeleza masomo yako katika Seminari ya Theologia ya Afrika Kusini (SATS) au Taasisi ya Theologia ya Argentina (FIET) unaweza omba nakala kwenye tovuti yetu na kubonyeza “Ombi ya Nakala”.
5) Ikiwa unataka kuomba Cheti cha Re-Forma kinachotolewa na Re-Forma pamoja na World Evangelical Alliance, hakikisha umekamilisha sehemu ya mwisho ya mtaala.
-
- Ni katika muundo wa daftari sehemu ya mwisho wa mtaala wa Live School.
- Unahitaji kusajili kwa kozi yandoa mtandaoni. Tazama maelezo katika daftari kwa mwongozo.
Baada ya kupakia ukurasa moja moja wa maandishi yanayohitajika, unaweza tuma ombi kwa kuenda kwa tovuti yetu na kubonyeza kwa; “Ombi la Cheti cha Re-Forma.”
Hadithi za hivi karibuni kutoka sehemu mbalimbali
Takwimu za Live School
Shule
Wanafunzi
Mataifa
Mtaala wa Live School
Live School ni mtaala uliokamilika na rahisi kubeba ya mafunzo ya misheni na mipango ya uanafaunzi. Inajumla ya mosomo 27 zilizoundwa na vipindi 242 vya saa moja ambazo vinatoa mafunzo kwa waumini asili na wenyeji ulimwenguni kote kama wamishenari wakimataifa ambao wanaweza panda makanisa yanayodumu na kuleta Injili kwa vikundi vya watu wao na Jirani.