Kuna mambo kadhaa unapaswa kuzingatia na kuamua kabla ya kuanza ratiba ya Live School. Ni kama yafuatavyo:
Kabla ya kutazama
1) Shule inaweza kufanyika “kwa mfululizo” au “ kwa muda”
-
- Katika shule ya mfululizo utahitajika kupitia vipindi vitatu kila siku, hii itachukua wiki 18 kukamilisha.
- Katika shule ya muda utahitajij miezi 18. Unaweza kuamua jinsi ya kupanga mtaala katika kipindi hiki.
- Njia bora ya kuendesha shule ni kukusanya pamoja kundi la wanafunzi, familia au marafiki ili wajiunge. Kwa njia hii utasaidia kufunza watu wengi zaidi kuwafikia waliopotea. Hata hivyo, umekaribishwa kusoma mtaala huu pekee yako, haswa kama unaishi kwenye nchi yenye uhasama au vikwazo.
- Kama una kundi, tafadhali uliza kila mmoja wao kujiandikisha kwenye portal ya Live School ili tuweze kudhibiti maendeleo yao.
- Ni bora kuwa na muda maalum uliotengwa wa Live School ili kila mmoja awe nayo kwenye ratiba yao.
- Njia nyingine ni kila moja wa kundi lako kutazama vipindi vya video kibinafsi, kwa kasi yao wenyewe na hatimaye kujadiliana pamoja.
Unapotazama
2) Mara kundi wakiwa wote pamoja, kuwa na wakati wa maombi na kisha onyesha/watazame video. (Ni muhimu kutazama kozi na vipindi kwa mpangilio uliowekwa diski mweko (thumb drive) kwa sababu maadili ya Live School hujijenga kanuni hadi kanuni, ambayo huchangia sana maendeleo ya mwanafunzi.
-
- Wakati unapotazama kipindi cha video, andika kile kilicho cha muhimu au kipepee kwako.
- Kipindi cha video kinapokamilika, uwe na muda majadiliano na kutafakari juu ya kile kila mmoja amejifunza. Himiza kila mmoja kuongeza pointi yoyote huenda walikosa katika maandishi yao.
- Unapoenda nyumbani, tumia maandishi yako, andika ukurasa moja wa kutafakari kwa mfumo wa mahubiri (katika pointi za viaridhishi/ufupisho)
- Kisha pakia ukurasa wako moja wa maandishi kwenye portal yako kwenye tovuti yetu. Unaweza kupiga picha kupakia. Kwa hivyo, hakuna haja ya kuitambaza.
- Weka maandishi yako ya ukurasa moja kwenye faili kama kumbukumbu na kwa matumizi ya baadaye.
- Endelea na mchakato huu hadi utakapokamilisha kozi.
Pindi unapokamilisha vipindi vyote vya Live School
3) Cheti cha ukamilisho wa Live School hutolewa baada ya maagizo haya kutimizwa:
-
- Umesoma na kukamilisha mtaala yote (masaa 242).
- Umepakia kurasa moja moja za maandishi kwenye portal yako.
- Umetuma ombi la cheti kwa kuenda kwa tovuti yetu na ukabonyeza kwenye “Ombi la Cheti cha Ukamilisho.”
4) Ikiwa unakusudia kuendeleza masomo yako katika Seminari ya Theologia ya Afrika Kusini (SATS) au Taasisi ya Theologia ya Argentina (FIET) unaweza omba nakala kwenye tovuti yetu na kubonyeza “Ombi ya Nakala”.
5) Ikiwa unataka kuomba Cheti cha Re-Forma kinachotolewa na Re-Forma pamoja na World Evangelical Alliance, hakikisha umekamilisha sehemu ya mwisho ya mtaala.
-
- Ni katika muundo wa daftari sehemu ya mwisho wa mtaala wa Live School.
- Unahitaji kusajili kwa kozi yandoa mtandaoni. Tazama maelezo katika daftari kwa mwongozo.
Baada ya kupakia ukurasa moja moja wa maandishi yanayohitajika, unaweza tuma ombi kwa kuenda kwa tovuti yetu na kubonyeza kwa; “Ombi la Cheti cha Re-Forma.”